Skip to content

Simba kujipongeza kwa nyama choma leo

NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba baada ya kutinga robo fainali za Kombe la Shirikisho la CRDB leo itakuwa na tamasha la nyama choma katika viwanja vya Gymkhana Jijini Arusha.

 Mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ulichezwa juzi kwenye Dimba la Sheikh Amri Abeid saa 10:00 Jioni.

 Katika mchezo huo Dodoma Jiji walitangulia kupata bao la kuongoza na baadae simba wakarudisha nakuongeza mabao mawili na kuwatupa nje ya mashindano wapinzani wao.

 Akizungumza na vyombo vya habari jana, meneja wa habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally alisema leo watakuwa na tamasha la nyama. 

Alisema wanasimba wote wanakaribishwa kwani watachoma na kula nyama za kutosha kwani kupokea Mbuzi wa kutosha kutoka kwa wadau na viongozi mbalimbali.

Mchezo wao unaofuata ni  ligi kuu ya NBC Tanzania Bara Aprili 15 dhidi ya Fountain Gate utachezwa Jijini hapo. 

Kikosi hicho kitarudi Dar es Salaam Aprili 16 kujiandaa na mchezo wao wa Aprili 18 Mkoani Lindi, Ruangwa dhidi ya Namungo FC.