NA MWANDISHI WETU KUCHEZA upatu imekuwa ni mtindo ambao wanawake wengi wamekuwa wakitumiakama njia ya ya kujikwamua kupata fedha au mtaji kwaajili ya kuendesha shughulimbalimbali za maisha yao ya kila siku. Wanawake saba katika kundi la wanawake 10 waliofanya mahojiano na makala haya wamewahikushiriki katika aina mbalimbali za upatu. Hata hivyo mtindo huo umekua ni fursa yenye tamu na chungu inayowakabili wanawake wengikutokana na changamoto za mfumo wa uendeshaji wake. Upatu upo aina mbalimbali kulingana na mfumo wa uendeshaji wake, kwa mfano upatu wa hisaambao ambao kundi la wanawake wanaungana katika kuweka kiasi kidogo kupata fursa ya kukopa kiwango maalumu bila riba ya marejesho. Pia kuna aina ya upatu unaohusisha vikundi vya ushirika, upatu wa vikundi vidogo vya uwekajina ukopaji kwa riba ambao maarufu mitaani kama (kausha damu), na nyengine. Upatu unafanyika katika maeneo ya kazi mfano maofisini, majirani, na hata kwa wanafamilia. Mtindo uliozoelekea zaidi upatu ni wa vikundi vidogo vya wasichana na wanawake katika maeneo ya makazi ambao wanaungana na kuweka utaratibu wa kuchangiana kiwango maalumucha pesa ambacho kila mshiriki atalamizika kutachangia kila baada ya muda. Vikundi hivi ambavyo mara nyingi inakuwa ni majirani, marafiki au familia vinakuwa na kiongozi maalumu anaechaguliwa miongoni mwa wanakikundi maarufu kama “kijumbe”.… Read More »Upatu: Mbinu yakujikwamua yenye tamu na chungu