WAKATI Ufaransa ikiendelea kupoteza kambi zake kadhaa za kijeshi barani Afrika, raiswa nchi hiyo, Emmanuel Macron, katika safari ya kimyakimya kwenye kituo cha mwishocha operesheni za nchi hiyo huko Djibouti, amekiri kwamba Afrika inapitia kwenyemabadiliko. Kwa mujibu wa rais huyo sababu kuwepo kwa mabadiko aliyoyashuhidia barani Afrika ni kutokana na maoni ya umma na serikali za nchi hizo na kueleza kuwa nafasi ya Ufaransa banihumo nayo lazima ibadilike. Katika safari hiyo, Macron amekiri kwamba kambi ya kijeshi ya Ufaransa nchini Djibouti inaweza kuwa na nafasi muhimu zaidi na kukiri kuwa Ufaransa inalazimika kubadilishamtazamo wake wa zamani dhidi ya uwepo wa majeshi yake barani Afrika. Macron pia ametangaza kuwa majukumu ya kambi ya kijeshi ya Ufaransa huko Djibouti yataangaliwa upya na kusema kambi hiyo inapaswa kutumika kama sehemu ya utumiaji nguvukatika baadhi ya misheni za Ufaransa barani Afrika.… Read More »Macron auona upande wa pili wa shilingi barani Afrika