MIAKA mitano iliyopita ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya nane ilikuwa na kishindo kikubwa cha mafanikio.
Chini ya utekeleza wa dira, mipango, mikakati na ilani ya uchaguzi ya 2025, serikali imepata mafanikio kwa kupiga hatua katika maeneo mbalimbali.
Katika makala haya, tuangalie kwa ufupi hatua za maendeleo zilizofikiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika sekta ya usafiri wa anga.
Kwa miaka kadhaa sekta ya usafiri wa anga imekuwa eneo muhimu sana kwa Zanzibar, hasa ikichukuliwa kuwa viwanja vya ndege vilivyopo visiwani hapa vinatumika kama milango rasmi ya kuingia na kutoka Zanzibar.
Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi, imechukua jitihada za kuhakikisha inaiimarisha sekta hiyo, ambapo hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na;
Serikali iliitafuta kampuni ya kimataifa kwa ajili ya DNATA kwa ajili ya kusimamia huduma za kiuendeshaji katika jengo la Terminal III la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Kutokana na uwekezaji huyo wa kampini ya DNATA, mapato yameongezeka kufikia shilingi bilioni 40.2 mwaka 2025 kutoka bilioni 12.9 mwaka 2021, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 211.6.
Ongezeko hilo la mapato kwa kiasi kikubwa limeonesha faida kwa uwekezaji huo ulivyokuwa na faida kwa kuongeza mapato serikalini.
Kiwanja hicho cha ndege, kimeshuhudia ongezeko la abiria kutoka 840,559 mwaka 2020 na kufikia 2,140,956 mwaka 2025.
Aidha kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume kimepokea tuzo ya kimataifa ya kuwa kiwanja bora Afrika kinachohudumia chini ya abiria 2,000,000.
Hatua nyengine zilizopigwa kwenye kiwanja hicho ni pamoja na kukamilika kwa kazi za awali za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Pemba wenye thamani ya euro milioni 170.
Kuendelea na ukarabati mkubwa wa jengo la abiria la Terminal II katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, ambao umefikia zaidi ya asilimia 57 ya ujenzi.
Kuimairisha ulinzi na usalama katika Viwanja vya Ndege vya AAKIA na Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa kununua na kufunga mashine za ukaguzi wa abiria na mizigo zikiwemo mashine tano za X-ray na ‘walk through metal detector’ 10 pamoja na mashine mbili za kukagulia miripuko – ETD.
Kuendelea kwa ukarabati mkubwa wa jengo la abiria la Terminal I ulioanza mwezi Mei mwaka 2024, ambao kwa sasa umefikia zaidi ya asilimia 84.
Ukarabati huo unahusisha huduma za wageni mashuhuri na mashuhuri zaidi, kumbi mbili za kuhudumia wageni kulingana na hadhi na madaraja yao pamoja na wageni mashuhuri wa kibiashara.
Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la abiria (eneo la kusubiria abiria) katika Uwanja wa Ndege wa Kigunda uliopo Nungwi.
Kuanza kwa ujenzi wa kituo cha biashara (business center) katika jengo la Terminal III na kuimarisha mazingira ya biashara katika Uwanja wa AAKIA kwa kuingia mkataba na Kampuni ya East Africa Developer
Limited kwa ajili ya kujenga na kuendesha kituo cha biashara (business center). Ujenzi huo unajumuisha jengo la maofisi, huduma za mabenki, maduka na mikahawa ambao umeshafika asilimia 56; na
Kuweka Mfumo Maalum wa kuongoza ndege wakati wa kutua (instrumental landing System – ILS) na uwekaji wa taa (Precision Approach Light) ambao humsaidia rubani kutua katika mazingira yote ya hali ya hewa.
