Skip to content

Buriani Raila Odinga Odinga

  • Makala

TAARIFA kutoka nchini Kenya, aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga amefariki akiwa na umri wa miaka 80, ambapo amefariki wakati akifanyiwa matibabu nchini India kulingana na duru za familia.

Odinga ambaye amemwacha mjane na watoto watatu ni mwanasiasa mashauhuri wa Kenya ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kuanzia 2008 hadi 2013.

Kabla ya kifo chake kiongozi huyo atakumbukwa kwa kupigania uhuru wa kidemokrasia, haki za kibinadamu na mabadiliko ya kitaifa.

Raila Odinga alikuwa mtu mashuhuri katika siasa za Kenya na Afrika, na kutia moyo kizazi chote barani.

Akiwa mwana wa mpiganiaji uhuru Jaramogi Oginga Odinga, makamu wa kwanza wa rais wa Kenya, Raila alisomea Ujerumani Mashariki kabla ya kurejea nyumbani miaka ya sabini.

Aliwekwa kizuizini kwa miaka sita baada ya kutuhumiwa kuhusika na jaribio la mapinduzi mwaka 1982 na baadaye alikamatwa tena kwa kushinikiza demokrasia chini ya utawala wa chama kimoja.

Alirejea kutoka uhamishoni baada ya kuanzishwa tena kwa siasa za vyama vingi kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge. Alikuwa na mchango mkubwa katika kukomesha utawala wa miongo kadhaa wa chama cha uhuru wa Kenya alipounga mkono jitihada za Mwai Kibaki za kuwania urais mwaka 2002.

Raila Odinga ambaye anajulikana sana kama Baba, aligombea urais mara tano, mara nyingi akiunganisha na kuunda upya upinzani, lakini hakuwahi kunyakua wadhifa huo wa juu zaidi.

Vita vyake vikali vilikuja kati ya mwaka 2007, wakati matokeo ya uchaguzi yaliogombaniwa kuzua ghasia nchi nzima, hatua iliosababisha makubaliano ya kugawana madaraka yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.

Safari ndefu ya kisiasa ya Raila Odinga, iliyojaa ukakamavu, ukaidi na kujitolea mhanga, ilimletea sifa ndani na nje ya nchi.

Wasifu wa Raila Odinga, kiongozi wa upinzani Kenya. Raila Amolo Odinga alizaliwa Januari tarehe 7 mwaka 1945 Magharibi mwa Kenya katika mkoa wa Nyanza.

Odinga, anayejulikana kwa wafuasi wake kama “Agwambo” kumaanisha mwenyekiti au mtu wa kushangaza kwa lugha yake asili ya jaluo, ni kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM). Ni kawaida kuwasikia wafuasi wake pia wakimuita ‘Baba’.

Aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa kwanza wa Kenya, wadhifa ulioundwa kufuatia Mkataba wa Kitaifa ulioafikiwa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, ambapo aligawana mamlaka na Rais Mwai Kibaki.

Alikuwa miongoni mwa viongozi watano wanaojiita Pentagon ambao wanaongoza muungano wa umoja wa vyama vya upinzani, National Super Alliance (NASA).

Kwenye muungano huo, anashirikiana na Kalonzo Musyoka (makamu wa rais wa zamani na kiongozi wa chama cha Wiper Democratic Movement -WDM), Musalia Mudavadi (makamu wa rais wa zamani na kiongozi wa chama cha Amani National Congress – ANC), Moses Wetangula (kiongozi wa chama cha Forum for Restoration of Democracy Kenya – Ford Kenya) na Isaac Ruto (kiongozi wa Chama cha Mashinani – CCM).

Kama hayati babake, Jaramogi Oginga Odinga, Raila aliishi kukamatwa na kuachiliwa mara kwa mara tangu mwaka 1982 hadi 1991 kwa harakati zake za kupigania mageuzi wakati wa muhula wa pili wa utawala wa rais Daniel arap Moi.

Kufuatia kuidhinishwa kwa katiba mpya, mwezi Agosti, mwaka 2010, amekuwa akisema kwenye kampeni zake kuwa nia yake ni kuleta mageuzi ya kisiasa na pia kumaliza ufisadi.

Odinga ni mwanasiasa anayesifika sana kwa ushawishi wake kisiasa na amekuwa katika msitari wa mbele kuunda vyama vya miungano na wanasiasa ambao ni mahasimu wake.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 1997 ambapo Raila alishikilia nafasi ya tatu, kufuatia kuundwa kwa muungano wa chama chake (NDP) na chama cha rais wa zamani Daniel moi (KANU), aliteuliwa kama waziri wa kawi katika serikali ya muhula wa mwisho wa Moi.

Mwaka 2002, baada ya Moi kumuunga mkono uhuru Kenyatta, kama mrithi wake, Raila na maofisa wengine wa KANU ikiwemo Kalonzo Musyoka na wafuasi wengine, walipinga ungwaji mkono wa Kenyatta kugombea Urais.

Waliungana na kiongozi wa upinzani Mwai Kibaki na na kuunda muungano wa National Rainbow Coalition (Narc) ambao baadaye ulishinda uchaguzi wa mwaka 2002.

Raila aliungana na Rais Mwai Kibaki kuunda serikali ya Muungano ya NARC baada ya kumuondoa mamlakani rais mstaafu Daniel Moi.

Mwaka 2005 aliungana na Uhuru Kenyatta aliyekuwa kama kiongozi rasmi wa upinzani, ili kushinda kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba chini ya serikali ya Rais Kibaki.

Wakati Kibaki alipomfuta kazi na washirika wake, aliunda chama cha ODM ambacho kilipiga kura ya ‘La’ dhidi ya rasimu ya katiba mpya ambayo ilishindwa mwaka 2005.

Aliongoza kampeni mwaka 2007 na kwa shingo upande kukubali ushindi wa rais Kibaki Katika uchaguzi uliokumbwa na utata, ghasia na mauaji.