Skip to content

Tupo tayari kucheza na Yanga Zanzibar  -Simba

NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

 MENEJA wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ali, amesema mechi yao na Yanga  kupelekwa uwanja wa  New Amaan Complex, Zanzibar  kwao sio tatizo kwani wanachotaka kushinda baada ya kupoteza dabi nyingi.

 Simba na Yanga zinatarajia kukukutana  Machi Mosi, Dimba la New Amaan Complex, saa 20:15 kwa saa za Afrika Mashariki.

 Mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam lakini wenyeji ambao ni Yanga wameuhamishia huko ambapo walitumia kucheza mashindano yao ya kimataifa.

 Akizungumza na gazeti hili jana Ahmed alisema wamepokea mabadiliko hawakuwa wameyatarajia lakini kwa kuwa yamefika hakuna shida wanajiandaa. 

Alisema haoni kama wapinzani wao wana bahati na uwanja huo kwani wangefanikiwa katika mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika.

 “Kwa sasa sio rahisi kuzungumzia maandalizi ya mchezo huo kwani tuna michezo miwili muhimu ya ligi ambayo itatupatia pointi sita hatuwezi kudharau pointi tatu kwa ajili ya mbili,” alisema 

Alisema raha ya dabi ni ushindi  Simba imepoteza michezo mingi ya dabi hivi karibuni , wanahitaji kushinda mchezo huo na  watajiandaa kwa hilo.