Skip to content

Mripuko wa gesi mgodini Nigeria waua 38

  • Blog

LAGOS, NIGERIA

WACHIMBA migodi 38 wamefariki wakati gesi iliporipuka kwenye shimo katikati mwa jimbo la Plateau nchini Nigeria, vyanzo vya ndani viliiambia AFP.

Taarifa zilisema kuwa watu wengine 27 walijeruhiwa katika mripuko huo wakiwa kwenye eneo la chini la uchimbani wa madini ya Kampanin Zurak huko wilaya ya Bashar katika jimbo la Plateau, kaimu mtawala wa kitamaduni aliiambia AFP.

“Hadi sasa watu 38 wamethibitishwa kufariki na wengine takriban 27 wamekimbizwa hospitalini,” alisema kiongozi huyo, Alhaji Aliyu Adamu Idris.

Ibrahim Dattijo Sani, mchimba madini katika shimo lililo karibu, aliiambia AFP kuwa wahasiriwa walikuwa chini ya ardhi katika mgodi ambapo mlipuko huo ulitokea kati ya saa 7:30 na 8:00 asubuhi kwa saa za huko.

“Tupo karibu na maeneo, watu walikuwa ndani ya mashimo ya madini na ghafla gesi iliripuka,” Sani alisema.