Skip to content

Wanachama Simba waonywa

NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

MENEJA wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amewataka wanasimba kuacha malumbano, ili kuirudisha timu kwenye utulivu na kujipanga kwa michezo ijayo.

Kikosi cha Simba kimewasili nchini jana baada ya kutoka sare ya bao 1-1dhidi ya Petro Atletico ya Angola ligi ya Mabingwa wa Afrika. 

Kikosi hicho kesho Februari 11 kitashuka dimbani dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa KMC Complex, uliopo Mwenge,Dar es Salaam, saa 1:00 usiku mchezo w aligi kuu Bara.

Akizungumza na vyombo vya habari jana, Ahmed Ally alisema malumbano ambayo yanafanyika hivi sasa kuikosesha utulivu timu yao kwani kuna baadhi ya wachezaji ni wageni na hawajazowea jambo ambalo linaweza kuwaweka wakati mgumu.

Alisema huu ni muda wa kuipa timu utulivu ili iweze kujipanga na kufanya vizuri hasa katika mashindano, ambayo yapo mbele yao, badala ya kila mtu kuzungumza lake na  kutoa ushauri kwa anacho kiona.

“Ni kweli tumefanya vibaya katika mashindano ya kimataifa na kutolewa kwenye hatua ya makundi hatujazowea matokeo ya namna hiyo, lakini hatuna budi kuyapokea kwani maisha ya kawaida mno kwenye mpira, mwaka huu tumefeli  mwakani tutashinda na kuna mwaka utakuja hata hatua ya makundi tutashindwa kufuzu,” alisema

Ahmed aliongea kwa msisitizo kuwa kujimilikisha uchungu na maumivu na kutoka hadharani kuzungumza mambo mengi kunaigawa timu na  kunaikosesha timu utulivu na kuwafanya wachezaji kuona Simba sio sehemu salama,hivyo hatuwezi kuwa na timu ya mpira ya namna hiyo.

 Katika hatua nyingine Ahmed alisema timu  imeingia kambini kwa kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya KMC.