Na Saida Issa, Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Malindi, Muhsin Haji Ussi ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Vijana kuweka fedha kwaajili ya mitaji rafiki kwa Vijana Nchini.
Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma ambapo amesema Vijana wanauthubutu ila changamoto waliyonayo ni kukosa mitaji na fedha.
“Vijana wanauthubutu, changamoto yao kubwa ni kukosa mitaji na fedha kwaajili ya kuendesha maisha yao katika kujiinua kiuchumi,”amesema
“Serikali imetoa asilimia 10% katika kila Halmashauri ambapo mapato yake yametengwa kwaajili ya kusaidia Vijana na kuwapa mikopo kina Mama na katika mikopo hiyo Vijana wanapata asilimia nne,”Amesema Muhsin
