WASHINGTON, MAREKANI
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema atamkaribisha kiongozi wa China Xi Jinping katika Ikulu ya White House mwishoni mwa mwaka huu, huku mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani yakitarajia kurejesha uhusiano uliokumbwa na vita vya kibiashara vinavyoendelea.
Trump alitoa maoni hayo katika mahojiano na NBC News yaliyorekodiwa wiki iliyomaliza siku hiyo hiyo yeye na Xi walikuwa na mazungumzo mapana kuhusu biashara, Taiwan, vita vya Urusi nchini Ukraine, na hali ya Iran.
Trump anatarajiwa kwenda China mwezi Aprili, kabla ya Xi kuzuru Marekani.
“Anakuja Ikulu ya White House, ndio — mwishoni mwa mwaka,” Trump alisema kwenye mahojiano hayo, ambayo sehemu ya mahojiano yake yalirushwa juzi Jumapili.
“Hizi ni nchi mbili zenye nguvu zaidi duniani na tuna uhusiano mzuri sana.” Alisema Trump.
Tangu Trump arejee Ikulu ya White House mwaka mmoja uliopita, amekuwa mfuatiliaji mahiri wa ushuru, akifichua tozo mahususi za sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na chuma, magari na bidhaa nyinginezo pamoja na hatua pana zaidi za kufikia malengo mbalimbali ya sera.
Ikulu ya White House imeshirikiana na Beijing kuhusu biashara lakini ikafikia mapatano mapana na Uchina baada ya kuongezeka kwa kiwango cha juu cha tozo mwaka jana.
Licha ya hatua kutoka Marekani iliyonuia kupunguza utegemezi wake kwa utengenezaji wa China, nchi hizo mbili zimesalia katika mshikamano mkubwa wa kiuchumi.
” Xi, ambaye alitembelea Marekani mara ya mwisho mwaka 2023, Jumatano alionya Trump kuendelea na “tahadhari” juu ya kuuza silaha kwa Taiwan inayojitawala, ambayo China inadai kuwa sehemu ya eneo lake.
Kiongozi huyo wa China pia alionyesha matumaini kuwa masuala ya pande mbili ikiwemo biashara yanaweza kutatuliwa kwa njia ya amani kati ya Beijing na Washington.
Siku ya Ijumaa, Marekani ilihimiza mazungumzo ya pande tatu na Urusi na China kuweka vikwazo vipya kwenye silaha za nyuklia, lakini Beijing hadi sasa imekataa kujiunga na mazungumzo hayo.
