Skip to content

Posts Archive

Waziri Haroun aeleza mkakati wa  kuimarisha mawasiliano, uchumi

  • Zanzibar

NA MWANAJUMA MMANGA WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawathamini wananchi wake ndio maana inaendelea kujenga barabara za kisasa ili kurahisisha mwasiliano na kuimarisha uchumi wao.   Waziri Haroun aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kidimni –Ubago, wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unmguja, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar. Alisema kufunguliwa kwa barabaraba hiyo kwa matumizi ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo kwani kutatanua wigo  na kuimarisha uchumi wa watu wa maeneohayo wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na kinamama pale wanaokwendakujifungua. “Bila shaka wananchi wa maeneo hayo wanajivunia na matunda ya mapinduzikwani kwao ni faraja hivyo ni vyema kuhakikisha tunaendeleza kutunzamiundombinu hiiili itusaidia kwa usafiri wa watu na mazao yanapoyatoamashambani. “Serikali ya awamu ya nane inayopongozwa na Rais wa Zanzibar… Read More »Waziri Haroun aeleza mkakati wa  kuimarisha mawasiliano, uchumi

Miundombinu ya kisasa  itaharakisha  upatinajaji haki – Dk. Shein

  • Zanzibar

RAIS mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya saba, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarishamiundombinu ya kisasa inayohakikisha wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria. Ameeleza hatua hizo ni pamoja na kujenga majengo ya kutosha ili kesi   zinazowasilishwa mahakamani zipate nafasi ya kuendeshwa na kutolewa mamuzikwa haraka zaidi  ili kupunguza mrundikano. Dk. Shein alieleza hayo wakati wa ufunguzi wa jengo la mahakama ya mkoa wa Kaskazini Unguja huko pale na kuongeza kuwa hapo awali mahakama ilikuwa na majengo finyu yaliyosababisha kuchelewa kutolewa kwa maamuzi hivyokuchelewesha upatikanaji wa haki kwa wananchi. Aidha rais huyo mstaafu alieleza kuwa inapendeza kuona sasa kuna majengomazuri na yenye nafasi pamoja na vitendea kazi watu jambo litakalochochea kasiya upatikanaji wa haki kwa wakati. “Huu ni ushahidi kwamba Zanzibar ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria inayojengwa kwa kuwepo mihimili mitatu ya serikali, Baraza la Wakilishi na Mahakama  ambayo ni misingi muhimu duniani katika utekelezaji wa utawalabora”, alieleza Dk. Shein. Aidha Dk, shein aliwataka wananchi kutumia mahakama kutoa ushahidi pale wanapohitajika ili kusaidia kupatika kwa haki kwani ushahidi ndio unaopelekeamtu kupata haki hivyo wananchi wasihofie. Vile vile aliwataka Majaji na Mahakimu kufuata sheria na kutoa haki kwa wananchi kwani jambo la haki limetajwa hata nadani ya vitabu vitukufu vya dini hivyo wanapaswa kuwa waadilifu. Naye Mtendaji Mkuu wa mahakama, Kai Bashir Mbarouk, akisoma ripoti  ya kitaalamu juu ya ujenzi huo , alisema… Read More »Miundombinu ya kisasa  itaharakisha  upatinajaji haki – Dk. Shein

Dk. Mwinyi: Tutajenga uwanja mfano wa  ‘Old Traford’

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujenga uwanja mkubwawa michezo wenye hadhi ya kimataifa, kitakachotumika kwa michuano ya kimataifaikiwemo michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027. Dk. Mwinyi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na wadau wa michezo waliohudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa viwanja vya michezoMaisara (Maisara Sports Complex), mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar. “Tuna dhamira ya kweli ya kujenga uwanja wa kisasa wa… Read More »Dk. Mwinyi: Tutajenga uwanja mfano wa  ‘Old Traford’