Skip to content

Mo Dewji anga’ra orodha ya matajiri wakubwa Afrika

  • Bara

MFANYABISHARA mashuhuri nchini Tanzania, Mohammed Dewji mwenye umri wa miaka 50, ameorodheshwa na jariba Forbes la nchini Marekani kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa 15 barani Afrika.

Katika orodha hiyo iliyotolewa Machi 9 mwaka huu, Mohammed Dewji ameshika nafasi ya 14 miongoni mwa matajiri wakubwa barani Afrika akiwa na kiasi cha dola bilioni 2.1 sawa na shilingi trilioni 5.4.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Mo Dewji katika nafasi hiyo anachuana na Strive Masiyiwa ambaye naye ameorodheshwa kuwa na kiasi cha dola 2.1 sawa na mfanyabishara huyo wa Tanzania.

Utajiri wa Mo Dewji unachangiwa na uwekezaji katika viwanda vya nguo, unga, mafuta ya kupikia, sabuni, sukari, vinywaji na biashara ya katani, akiwa ameajiri watanzania patao 25,000.

Katika Unkanda wa Afrika Mashariki, Mo Dewji wamekuwa mfanyabishara pekee katika kanda hiyo kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wenye utajiri mkubwa barani Afrika akiwa chini ya umri wa miaka 60

Mfanyabiashara huyo ni chachu ya kukua kwa MeTL ambapo shughuli zake zimetanuka katika nchi za Afrika zisizopungua 10 zikiwemo Uganda, Ethiopia na Kenya.

Mfanyabiashara huyo mwaka 2016, alitoa ahadi ya kutumia nusu ya utajiri wake katika kutoa uhisani na ufadhili wa kuboresha huduma za kijamii na zinazochochea maendeleo na shughuli za kijamii.

Nafasi ya kwanza ya tajiri mkubwa barani Afrika imeendelea kushikiliwa na raia wa Nigeria, Aliko Dangote anayemiliki viwanda vya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali akiwa na utajiri wa kiasi cha dola milioni 28.5.

Mo Dewji pamoja na kuwa Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba, ndiye mwekezaji wa klabu hiyo ambaye amewekeza shilingi bilioni 21, huku akisubiri mchakato wa maaadiliko ya klabu hiyo kukamilika.

Taarifa za jarida hilo zilieleza kuwa katika mwaka 2025, tajiri huyo nambari moja barani Afrika, aliweka rekodi ya kupata faida kwenye biashara zake kwa kuingiza kiasi cha neira (fedha za Nigeria) trilioni moja.

Huku nafasi ya pili ikichukuliwa na familia ya Johann Rupert ambayo inajishughulisha na biashara za mitindo ya mavazi akiwa na utajiri wa dola milioni 16.1, ambapo mfanyabishara wa bidhaa mchanganyiko Abdulsamad Rabiu akishika nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa dola 11.2.

Nafasi ya nne imechukuliwa na familia ya Nicky Oppenheimer inayojihusisha na biashara ya madini ikiwa na utajiri wa dola bilioni 10.6, huku Nassef Sawiris akishika nafasi ya tano akiwa na utajiri wa dola bilioni 9.6.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliomo kwenye orodha hiyo ni pamoja na rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe anayejishulisha na biashara ya madini akiwa na utajiri wa kiasi cha dola 4.3.