Na Saida Issa, Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Martha Gido ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, akisema miradi hiyo imekuwa na tija ya moja kwa moja kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Akichangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo nje ya viwanja vya Bunge jijini Dodoma, mbunge huyo alisema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inaonekana wazi katika utekelezaji wake, kwani inalenga kumuwezesha mwananchi kiuchumi na kijamii bila kumuacha mtu nyuma.
Alieleza kuwa miradi inayotekelezwa imegusa makundi yote ya jamii yakiwemo watoto, wazee, wanawake na vijana, hali inayothibitisha kuwa Serikali inazingatia maendeleo jumuishi kwa Watanzania wote.
“Serikali hii ya Mama Samia imeonesha kwa vitendo kuwa ikiahidi inatekeleza. Si maneno, bali matendo yanayogusa maisha ya wananchi,”alisema.
