RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na viongozi wa serikali, wapiganaji vikosi vya Ulinzi na Usalama, wanafamilia na wananchi katika maziko ya Bi Sichana Is-haka Daima, aliyefariki jana.
Marehemu Bi Sichana Daima alifariki jana alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa Lumumba, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Maziko hayo yamefanyika huko Bumbwini, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Marehemu Sichana Is-haka Daima ni mama mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kanali Makame Abdallah Daima.
Awali hapo jana Dk. Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya kiislamu katika swala ya jeneza iliyosaliwa katika msikiti wa Bumbwini Misufini.
Marehemu Sichana Is-haka Daima amezikwa kijijini kwao Bumbwini Hasara Roho, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi.

