Skip to content

Kitaifa

Dk. Mwinyi anogesha furaha Zanzibar Heroes 

NA KHAMISUU ABDALLAH  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajia kuunda kamati maalum ya kumshauri namba bora ya kukuza soka la Zanzibar.  Dk. Mwinyi alieleza hayo katika hafla ya chalula cha mchana aliyoiandaa kwa ajili yakuwapongeza mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup timu ya Taifa ya Zanzibar,… Read More »Dk. Mwinyi anogesha furaha Zanzibar Heroes 

Dk. Mwinyi: Mazoezi kinga madhubuti ya maradhi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyiamewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kufanya mazoezi kwani ni kinga madhubutidhidi ya maradhi hasa yasioambukiza. Dk. Mwinyi aliyasema hayo katika viwanja vya Mnazimmoja Wete wakati akizungumza nawananchi waliojikeza katika bonanza la mazoezi kitaifa lililoambata na na matembeziyaliyoanzia katika uwanja wa mpira Kinyasini hadi uwanja wa Mnazimmoja, Wete Pemba. Alieleza kuwa kufanya mazoezi kutaweza kupunguza na kuondosha maradhi yasioambukizayakiwemo ya kisukari, presha pamoja na unene uliyokithiri. Aidha Dk. Mwinyi alifahamisha kuwa kuwa maradhi yasioambukiza yamekuwa yakiongezekasiku hadi siku yakilinganishwa na maradhi yanayoambukiza ambayo yalikuwa yakiongoza katikamiaka iliyopita. “Niwaombe sana ndugu wananchi, tusiache kufanya mazoezi kwani kufanya mazoezikunapelekea kujikinga na maradhi yasioambukiza,  hili tuelewe wazi”, alieleza Dk. Mwinyi. “Lakini pia niwafahamishe wana michezo wenzangu kuwa mazoezi ni afya, hivyo tuendeleekufanya mazoezi ili tuweze kuweka miili yetu sawa”, alieleza Dk. Mwinyi. Sambamba na hayo Rais Mwinyi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha hali ya amani, umoja na utulivu uliopo nchini hasa katika kipindi hiki nchi ikielekea katika uchaguzimkuu hapo baadae. “Niwaombe sana viongozi wa dini na wanasiasa kuendelee kuwahubiria wafuasi wetu juu ya umuhimu wa kuitunza amani ya nchi iliyopo”, alisisitiza Dk. Mwinyi.  Mapaema Dk. Mwinyi aliupongeza uongozi wa Chama cha Wafanya Mazoezi Zanzibar (ZABESA) kwa kuwashajihisha wananchi kuendelea kufanya mazoezi pamoja na kuendelezasiku ya mazoezi kitaifa nchini. Aidha… Read More »Dk. Mwinyi: Mazoezi kinga madhubuti ya maradhi

Waziri Haroun aeleza mkakati wa  kuimarisha mawasiliano, uchumi

  • Zanzibar

NA MWANAJUMA MMANGA WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawathamini wananchi wake ndio maana inaendelea kujenga barabara za kisasa ili kurahisisha mwasiliano na kuimarisha uchumi wao.   Waziri Haroun aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kidimni –Ubago, wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unmguja, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar. Alisema kufunguliwa kwa barabaraba hiyo kwa matumizi ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo kwani kutatanua wigo  na kuimarisha uchumi wa watu wa maeneohayo wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na kinamama pale wanaokwendakujifungua. “Bila shaka wananchi wa maeneo hayo wanajivunia na matunda ya mapinduzikwani kwao ni faraja hivyo ni vyema kuhakikisha tunaendeleza kutunzamiundombinu hiiili itusaidia kwa usafiri wa watu na mazao yanapoyatoamashambani. “Serikali ya awamu ya nane inayopongozwa na Rais wa Zanzibar… Read More »Waziri Haroun aeleza mkakati wa  kuimarisha mawasiliano, uchumi