Miundombinu ya kisasa itaharakisha upatinajaji haki – Dk. Shein
RAIS mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya saba, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarishamiundombinu ya kisasa inayohakikisha wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria. Ameeleza hatua hizo ni pamoja na kujenga majengo ya kutosha ili kesi zinazowasilishwa mahakamani zipate nafasi ya kuendeshwa na kutolewa mamuzikwa haraka zaidi ili kupunguza mrundikano. Dk. Shein alieleza hayo wakati wa ufunguzi wa jengo la mahakama ya mkoa wa Kaskazini Unguja huko pale na kuongeza kuwa hapo awali mahakama ilikuwa na majengo finyu yaliyosababisha kuchelewa kutolewa kwa maamuzi hivyokuchelewesha upatikanaji wa haki kwa wananchi. Aidha rais huyo mstaafu alieleza kuwa inapendeza kuona sasa kuna majengomazuri na yenye nafasi pamoja na vitendea kazi watu jambo litakalochochea kasiya upatikanaji wa haki kwa wakati. “Huu ni ushahidi kwamba Zanzibar ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria inayojengwa kwa kuwepo mihimili mitatu ya serikali, Baraza la Wakilishi na Mahakama ambayo ni misingi muhimu duniani katika utekelezaji wa utawalabora”, alieleza Dk. Shein. Aidha Dk, shein aliwataka wananchi kutumia mahakama kutoa ushahidi pale wanapohitajika ili kusaidia kupatika kwa haki kwani ushahidi ndio unaopelekeamtu kupata haki hivyo wananchi wasihofie. Vile vile aliwataka Majaji na Mahakimu kufuata sheria na kutoa haki kwa wananchi kwani jambo la haki limetajwa hata nadani ya vitabu vitukufu vya dini hivyo wanapaswa kuwa waadilifu. Naye Mtendaji Mkuu wa mahakama, Kai Bashir Mbarouk, akisoma ripoti ya kitaalamu juu ya ujenzi huo , alisema… Read More »Miundombinu ya kisasa itaharakisha upatinajaji haki – Dk. Shein










