Skip to content

Dk. Samia kulipa mshahara wa kocha Taifa Stars

NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda amesema  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan atalipa  mshahara wa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Akizungumza na vyombo vya habari jana wakati wa ukaguzi wa wa maendeleo ya uimarishaji wa uwanja wa Benjamini Mkapa kuelekea kwenye AFCON 2027,Makonda  alisema taratibu zote za kocha Miguel Ángel Gamondi kusaini mkataba zimekamili kwa upande wa Serikali, BMT na imebakia TFF kukamilisha utaratibu. 

Makonda alilisisitiza kuwa Rais Dk. Samia ndiye atamlipa kocha huyo na ameamua kuwekeza na kuhakikisha kocha Gamondi anaendeleza kufanya vyema ili kukamilisha ndoto ya watanzania wengi kombe la Afcon 2027 kubakia Tanzania. 

Alisema mbali na utaratibu huo lakini wamepokea maombi mengi ya makocha ambao wanataka kuinoa Taifa Stars, lakini maamuzi ya serikali  ni kubakia na kocha  ambaye ameanza na anawafahamu wachezaji lakini hata wachezaji wanamfahamu. 

“Gamondi amepewa timu katika muda mfupi lakini amefanya mambo mazuri, hivyo hakuna sababu ya kutafuta kocha mpya, ambaye atakuja kuanza tena kwani wachezaji wamemzowea”alisema.

 Gamondi mwaka jana alikabidhiwa timu hiyo ambayo ilikuwa chini ya kaimu kocha mkuu Hemed Selemani ‘Morocco’ na kufanikiwa kuivusha kwenye hatua ya robo fainali za AFCON 2025 nchini Morocco.