Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameondoka nchini kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) leo tarehe 02 Februari, 2026, ambapo atashiriki kwenye mkutano wa World Government Summit (WGS 2026) na uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS).
Mkutano wa WGS 2026, unaobeba kaulimbiu “kutengeneza serikali zijazo (Shaping Future Governments)”, ni jukwaa la kimataifa linalowakutanisha wakuu wa nchi na serikali, watunga sera, viongozi wa taasisi za kimataifa, sekta binafsi na wawekezaji wakubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Vilevile, Rais Samia atashiriki uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS), jukwaa la kimkakati la uwekezaji lililoanzishwa na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa.
#Zanzibarleo
