Skip to content

JKT latangaza nafasi za kjitolea kwa vijana

  • Bara

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza nafasi za mafunzo ya kujitolea huku likisisitiza hakuna gharama yoyote kupata nafasi hizo isipokuwa zinatolewa kwa wale waliokidhi vigezo.

‎Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena aliwataka wazazi wawe macho dhidi ya matapeli wanaotumia nafasi hizo kujinufaisha.

‎”Tunapotangaza nafasi hizi, baada ya muda huwa tunapigiwa simu na kupata taarifa kuna baadhi ya wazazi wametoa pesa kupata nafasi lakini hawajapata, nasisitiza nafasi hizi ni bure”, alisema Mabena.

‎‎Aidha alisema nafasi hizo zimepelekwa kwenye ofisi za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchi nzima ambapo usajili utafanyika kuanzia Januari 26 na watakaochaguliwa wanatakiwa kuripoti Makambi ya JKT kuanzia Februari 27 Hadi Machi 4, mwaka huu.

‎‎Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Mabena, JKT linawataarifu vijana watakaopata nafasi za mafunzo hayo ya kujitolea kwamba, halitoi ajira wala halihusiki kuwatafutia ajira sehemu yoyote Ile.

‎‎”Sifa na vifaa vya kwenda navyo makambini vinapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz”alisema Brigedia Jenerali Mabena.