ANTANANARIVO, MADAGASCAR
JESHI la Madagascar limechukua udhibiti wa kisiwa cha Bahari ya Hindi, kanali wa jeshi alisema Jumanne, baada ya Rais Andry Rajoelina kutoroka nje ya nchi wakati wa mzozo na waandamanaji wanaoongozwa na vijana na vikosi vya usalama.
“Tumechukua mamlaka,” Kanali Michael Randrianirina, ambaye aliongoza maasi ya wanajeshi waliojiunga na waandamanaji wanaoipinga serikali, alisema kwenye redio ya taifa.
Randrianirina aliongeza kuwa jeshi lilikuwa likizivunja taasisi zote isipokuwa bunge la chini au Bunge la Kitaifa, ambalo lilipiga kura ya kumshtaki Rajoelina dakika chache mapema.
Katika siku ya machafuko kwa taifa hilo lililo nje kidogo ya Afrika mashariki, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 51 alikuwa ametaka kulivunja bunge hilo kwa amri.
Licha ya kuruka kwa ndege ya kijeshi ya Ufaransa, Rajoelina anakataa kuachia ngazi kwa wiki kadhaa za maandamano ya GenZ wanaomtaka ajiuzulu na kuenea kwa uasi katika jeshi.
Ofisi ya rais haikujibu mara moja maoni ya Randrianirina lakini mapema ilisema mkutano wa bunge ulikuwa kinyume cha katiba na hivyo azimio lolote ni batili.
