KHARTOUM,SUDAN

POLISI  nchini Sudan wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokusanyika kwa wiki ya nne kutaka kuondoka uongozini kwa Rais Omar al-Bashir.

Bashir amekuwa madarakani kwa miongo mitatu sasa. Maandamano yaliyochochewa na mzozo wa kiuchumi yameitikisa Sudan tangu katikati ya mwezi Disemba hatua ambayo imemuumisha kichwa zaidi Bashir katika uongozi wake.

Wanaharakati wanasema maandamano yamefanyika katika miji ya Gadarif, Faw na Amri pamoja na eneo la magharibi la Darfur. Walioshuhudia wanasema polisi wameyavunjilia mbali maandamano makubwa ya watu elfu moja katika mji wa el-Fasher ulioko kaskazini mwa Darfur.

Maandamano ya Darfur yalianza mwezi uliopita ambapo yalichochewa na kuongezeka mara tatu kwa bei ya mkate.

MAONI YAKO