NA MWANDISHI WETU

MASHINDANO ya mpira wa mikono mapinduzi cup 2019 yamehitimishwa rasmi kisiwani Pemba baada ya kupatikana washindi wa nne wa mchezo huo.

Akizugumza wakati akifunga mashindano hayo Naibu waziri nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum (SMZ) pia ni mwakilishi wa Micheweni Shamata Khamis, amesema jitihada za makusudi zinahitajika ili kukuza mchezo huo kuanzia ngazi za watoto ili kuwa na wachezaji wengi kwenye mchezo huo.

Aidha ameiomba serikali ya SMZ kuhakikisha wanaweka inawapa kipaumbele michezo mingine nje ya soka ambayo inaweza kuiwakilisha vizuri nchi kwenye mashindano ya kimataifa na kuitangaza nchi yetu kwenye nyanja zote.

‘’Mchezo huu umekuja kuleta changamoto hapa kisiwani Pemba upo chini sana tofauti na mpira wa miguu, sasa tunakwenda kuanza mchezo huu rasmi kisiwani Pemba’’ Alisema Shamata.

Kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo pia ni mjumbe wa ZAHA Kombo Ali amesema mashindano hayo yamefanyika yakiwa na changamoto kubwa ya udhamini.

‘’Mchezo huu ni wa wazi hauna vingilio kwa hapa kwetu sasa tunaiomba sana serikali na wadau wengine wa mpira wa mikono inatuunga mkono’’ alieleza Kombo.

Katika mashindano hayo timu ya Ngome wanaume na wanawake  kutoka Tanzania bara wamefanikiwa kutwaa ubingwa, wakati kwa upande wa vijana  mshindi wa kwanza Data kutoka Tanga na kwa wanawake klabu ya Uzini.

MAONI YAKO