KAMPALA,UGANDA

WATU  16 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baaada ya gari walilokuwamo kupinduka katika eneo la kilima wilaya ya Pakwach.

Abiria waliokuwamo katika gari hiyo aina ya  Fuso, wengi wao wakiwa ni wafanyabiashara waliokuwa wakisafiri kutoka Ariwara mashariki mwa Congo  mapakani na wilaya ya Arua wakielekea katika soko la  Panyimur kwa ajili ya kununua samaki.

Soko hilo ni mashuhuri kwa wafanyabiashara wa aina mbalimbali za samaki. Kwa mujibu wa polisi, tukio hilo lilitokea baada ya dereva wa Fuso lililobeba idadi kubwa ya watu, kukosa uelekeo na kushindwa kulidhibiti gari kilomita mbili kutoka soko la  Panyimur.

Msemaji wa polisi  West Nile,  Josephine Angucia, alithibitisha ajali hiyo na kusema kwamna waliofariki wengi wao walikuwa ni wafanyabiashara kutoka  Ariwara Congo.

MAONI YAKO