TUNIS, TUNISIA

MAHAKAMA nchini Tunisia imewahukumu kunyongwa watu 41 waliokuwa wakituhumiwa kutekeleza shambulio la kigaidi nchini humo.

Sufyan al Saliti msemaji wa vyombo vya sheria vya kupambana na ugaidi nchini Tunisia ameeleza kuwa mahakama ya wilaya nchini humo imewahukumu kunyongwa magaidi 41.

Ameongeza kuwa, hukumu hiyo iliyotolewa inawahusu watuhumiwa waliohusika katika shambulio la mwezi Januari mwaka 2014 dhidi ya askari walinzi wa mpakani, ambapo 15 miongoni mwa askari hao waliuawa.

Msemaji wa vyombo vya sheria vya kupambana na ugaidi nchini Tunisia amesisitiza kuwa watuhumiwa wote katika kesi hiyo ni wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh.

MAONI YAKO