NEW YORK, MAREKANI

KUFUNGWA  kwa shughuli za serikali ya Marekani kulikosababishwa na msimamo wa rais Donald Trump wa kutaka kiasi cha dola Bilioni 5.7 kwa ajili ya kujenga ukuta kati ya nchi yake na Mexico umeingia katika siku ya 23, na hivyo kuvunja rekodi katika historia ya Marekani.

Mkwamo huo ulioanza Desemba 22 mwaka uliopita hauonyeshi dalili ya kumalizika. Trump ameonya kwamba mkwamo huo unaweza ukawa mrefu zaidi na amewalaumu Wademokrats kwa kuusababisha.

Kwa upande wao Wademokrats wanasema Rais Trump ndiye aliyesababisha mkwamo huo kutokana na kiburi chake na kukataa kutia saini sheria iliyopitishwa na vyama vyote viwili mwaka uliopita ambayo haikujumuisha fedha kwa ajili ya ukuta huo.

MAONI YAKO