YEREVAN, ARMENIA

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan ametangaza kujiuzulu kwake miezi sita baada ya kuwa afisini.

Pashinyan anataka kulazimisha kufanyike uchaguzi mpya wa bunge mwezi Desemba.

Katika tangazo kwenye televisheni Pashinyan amesema Armenia inakwenda katika hatua mpya na kwamba mageuzi ya amani yaliyofanyika nchini humo yanastahili kufikishwa mwisho.

Pashinyan alichaguliwa na bunge kama kiongozi wa serikali mwezi Mei baada ya maandamano ya wiki kadhaa.

Lakini bunge bado lina idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha rais wa awali Serzh Sargsyan, jambo lililofanya kazi ya serikali ya Pashinyan kuwa ngumu.

MAONI YAKO