KIGALI,RWANDA

MKURUGENZI  wa mamlaka ya maendeleo ya uchimbaji wa madini ya Rwanda amesema,  Rwanda inatafuta wawekezaji zaidi katika sekta ya madini, ili kuhimiza uuzaji wa madini nje na kuongeza mapato.

Ofisa mkuu mtendaji wa Bodi ya madini, mafuta na gesi ya Rwanda Bw. Francis Gatare, amesema Rwanda ikiwa ni moja ya nchi zinazoendelea kwa kasi kiuchumi barani Afrika, kutokana na maliasili yake ya madini, ina fursa nzuri ya kuhimiza maendeleo ya sekta ya viwanda, na mageuzi ya kiuchumi kwa pande zote.

Ameongeza kuwa sekta ya madini ya Rwanda inatoa fursa tofauti kwa wawekezaji, ikiwa ni pamoja na kutafuta na kuchimba madini, kuongeza thamani na kupata mafunzo ya sekta ya viwanda. Rwanda inalenga kupata dola milioni 800 za kimarekani kabla ya mwaka 2020, na dola bilioni 1.5 za kimarekani kabla ya mwaka 2024 kutokana na uuzaji wa madini nje ya nchi.

MAONI YAKO