KAMPALA, UGANDA

JESHI la Polisi nchini Uganda limetaka mwanamuziki mashuhuri nchini humo  Robert Kyagulanyi maarufu kama  Bobi Wine,  kuakhirisha tamasha la muziki alililopanga kufanya katika uwanja wa taifa wa  Namboole  siku ya Jumamosi.

Katika barua iliyojibu kwa Meneja wa  Emma Promosheni  na  masoko ,  Emma Serugo, ambaye aliomba kupatiwa ulinzi wakati wa tamasha hilo,  Asuman Mugyenyi, Mkuu wa operesheni za polisi alisema uongozi wa uwanja wa  Namboole hawana taarifa za tamasha la muziki litakalofanywa na Mbunge wa  Kyadondo Mashariki, Bobi Wine.

“Uongozi wa uwanja wa mpira wa Taifa Namboole umetuthibitisia kuwepo kwa shughuli mbalimbali zilizopangwa kufanyika uwanjani hapo kuanzia Septemba  2018 hadi Januari  2019 lakini hakukuwa na orodha ya kuwepo kwa tamasha la muziki ambalo ni uzinduzi wa albamu ya Kyarenga . Kwa hivyo mnashauriwa kuakhirisha tamasha kwa vile hamkufanya matayarisho na uongozi wa Mandela kwa ajili ya Oktoba 20, 2018,” ilisomeka sehemu ya barua iliyoandikwa kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa wa Polisi,  Martins Okoth-Ochola.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Bobi Wine kurejea kutoka Kenya na kuelezea taharuki yake juu ya Jeshi la Polisi Uganda kushindwa kueleza iwapo tamasha la muziki alilopanga kulifanya ni halali au la.

Bobi Wine amesema, uongozi wa Jeshi la Polisi Uganda umekuwa ukionekana kuchafua mipango yake kwa kutoa maoni ambayo hayaeleweki kwa timu yake

MAONI YAKO