NORTH IRELAND

Mwandishi wa Fasihi wa Ireland Kaskazini Anna Burns amepokea tuzo maarufu ya Man Booker Prize kwa fasihi ya lugha ya Kiingereza.

Burns mwenye umri wa miaka 56 ametuzwa kutokana na kitabu chake kwa jina “Milkman”.

Kitabu hicho kinaeleza kuhusu msichana mwenye umri wa miaka 18 kutoka Ireland Kaskazini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo anaeleza kuhusu udhalilishaji wa kingono aliopitia, mzozo na matatizo ya kijamii.

Tuzo hiyo ya Man Booker Prize ilianza kutolewa tangu mwaka wa 1969 na iliwaendea pia waandishi wengine kama Margaret Atwood na Salman Rushdie.

MAONI YAKO