NEW YORK, MAREKANI

Ripoti ya idadi ya watu duniani ya mwaka 2018 inaonyesha kuwa kila mwanamke duniani leo anajifungua wastani wa watoto 2.5.

Idadi hiyo ni kama nusu chini ya ilivyokuwa katikati ya miaka ya 1960.

Katika mataifa yaliyoendelea kiviwanda, ripoti hiyo imeonyesha kwamba mwanamke anazaa watoto wachache kuliko inavyotakiwa duniani.

Katika mataifa maskini duniani matokeo ni kinyume ya hicho. Kati ya mataifa 43 ambayo wanawake wanazaa angalau watoto wanne, mataifa 38 ni ya Afrika.

Ripoti hiyo inasema idadi hiyo kubwa ya uzazi inatokana na ukosefu wa elimu na kinga wakati wa ngono.

MAONI YAKO