ADDIS ABABA,ETHIOPIA

WAZIRI  Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali , amemteua mwanamke Muislamu  kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, ikiwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo.

Abiy Ahmed Ali amemteua Aisha Mohammed kuwa Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia.  Waziri Mkuu wa Ethiopia amebadilisha mawaziri 16 katika serikali ya nchi hiyo na kupunguza idadi ya wizara ya serikali kutoka 28 hadi 20. Nusu ya mawaziri wapya wa baraza la mawaziri la Ethiopia inaundwa na wanawake.

Chama tawala nchini Ethiopia kilimchagua Abiy Ahmed Ali kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo baada ya kujiengua waziri mkuu wa zamani, Hailemariam Desalegn ambaye kipindi cha uongozi wake kiliandamana na ukandamizaji mkubwa wa wapinzani wa serikali.

Awali Bunge la Ethiopia lilikuwa limechukua hatua ya aina yake nchini humo na kumteua mwanamke Muislamu, Muferiat Kamil kuwa spika wa bunge hilo. Hata hivyo Bi Muferiat Kamil alijiuzulu nafasi hiyo siku chache zilizopita na kuteuliwa kama Waziri wa Amani.

MAONI YAKO