NA MWANDISHI WETU

TIMU Taifa ya Tanzania Taifa Star jana iliweka hai matumaini ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) , ambapo fainali yake itachezwa mwakani nchini Cameroon, baada ya jana kuifunga timu ya taifa ya Cape Verde mabao 2-0.

Mchezo huo wa marudiano ulipigwa katika dimba la taifa majira ya saa 11:00 jioni, ambapo mchezo wa awali ulipigwa nchini  Cape Verde ambapo stars ililala kwa mabao 3-0.

Star ilishuka uwanjani ikiwa na deni kubwa kwa Watanzania ambapo jana dhahiri ilionekana kurekebisha makosa ya mchezo wa kwanza, na walicheza kwa umakini mkubwa hivyo kufanikiwa kutoka na ushindi huo.

Mchezo huo ulianza kwa kila upande kutafuta bao la kuongoza ili kujiweka mazingira mazuri ya kutoka na ushindi, ambapo Star ilipata bao la kwanza dakika ya 29 bao lililofungwa na Simon Msuva, kufuatia kazi nzuri ya Samatta na Msuva kumalizia kufunga bao safi.

Stars ingeweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, lakini mkwaju wa penalti wa nahodha Mbwana Samatta, uligonga mwamba na kurejea uwanjani kabla ya kuokolewa.

Baada ya bao hilo timu hizo ziliendelea kushambuliana Cape Verde ikitaka kusawazisha na Star ikisaka bao la pili, lakini hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Star ilitoka na ushindi wa bao moja.

Kipindi cha pili mchezo huo ulizidi kuwa mkali zaidi kwani kila timu kujipanga na kushambulia lango la mwenzake, lakini kwa mara nyingine tena Star ikafanikiwa kutumia nafasi walioipata kwa kuandika bao la pili lilifungwa na Mbwana Samata.

MAONI YAKO