KAMPALA, UGANDA

WAZIRI wa nchi katika masuala ya Afya ya awali ,  Joyce Moriku Kaducu amewaonya Waganda kuacha tabia ya kutumia dawa za asili kutibu maradhi ya macho akieleza kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini  Kampala, Dkt.  Kaducu aliwataka wale wote wenye matatizo ya macho kuonana na wataalamu wa macho kwa ajili ya kupata matibabu sahihi.

“Macho ni sehemu zinazohitaji uangalifu sana katika mwili wa mwanadamu. Dawa za mitishamba haziwezi kusaidia, zinaweza kuathiri uoni wako,” alieleza Dkt. Kaducu.

Alisema matatizo ya macho yanatokana na mazingira machafu, kutazama televisheni wakati taa zimazimwa, kusoma katika mwaga hafifu , uvutaji sigara na matumizi ya mkojo ni miongoni mwa mambo yanayochangia tatizo.

“Vilivyomo kwenye mkojo si salama kuingizwa machoni kwa sababu mkojo una aside na hairuhusiwi kamwe. Mkojo umethibitishwa kwamba hauwezi kutibu matatizo ya macho,” alifahamisha Dkt.  Kaducu.

Aidha aliwataka Waganda kujipumzisha mara kwa mara wakati wanaposoma au kutazama televisheni na pia kufanya vipimo mara kwa mara.

MAONI YAKO