RAHEEM STARLING
REAL Madrid inafuatilia hali ya Raheem Sterling huko Manchester City kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 wa England ataingia miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake. (ESPN).

AARON RAMSEY
LIVERPOOL na Manchester United wanapima uzito wa bei uhamisho wa Januari kwa kiungo wa Arsenal na Wales, Aaron Ramsey (27). (London Evening Standard).

JORDI ALBA
MANCHESTER United inazingatia kufanya jitihada kwa mlinzi wa Barcelona na Hispania, Jordi Alba (29). (Mundo Deportivo).

JESSE LINGARD
MANCHESTER United wataanzisha mazungumzo mapya ya mkataba na kiungo wa England, Jesse Lingard (25), katika wiki zijazo. (Metro).

NICOLAS PEPE
KLABU za Arsenal na Manchester United zitapambana na ushindani kutoka Bayern Munich katika kusajili winga wa Lille na Ivory Coast, Nicolas Pepe (23). (Bild).

LUCAS PAQUETA
AC Milan amezishinda Liverpool na Manchester United kwa saini ya kiungo wa Brazil wa Flamengo mwenye umri wa miaka 21, Lucas Paqueta. (Sun).

MAONI YAKO