Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola (CTE) Mangina, Kivu Kaskazini, DRC.

JUBA, SUBAN KUSINI

WAFANYAKAZI wa Afya waliopo katika jimbo la Tambura wamesema, eneo hilo bado lipo hatarini na mripuko wa Ebola wakieleza kutokea kwa visa vipya katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), hadi  Oktoba 7, kumekuwepo na kesi  181 za Ebola wakati vifo 11e vikiripotiwa kutoka vituo tisa vya Afya vikiwemo Mabalako na  Beni.

Baada ya mripuko mpya mwezi uliopita, Wizara ya Afya ya Sudan Kusini na wadau wake walianzisha kampeni kubwa za uhamasishaji  katika jimbo la Ekwetoria ambalo lipo mpakani na DRC.

Waziri wa Afya Tambura,  David Simbi alieleza kwamba vituo vyote vya mpakani na Congo vimefungwa isipokuwa kwa maeneo yenye vifaa vya uchunguzi ili kuzuia uwezekano wa kuenea kwa Ebola.

Simbi alifahamisha kuwa hakuna kesi iliyoripotiwa lakini onyo limetolewa kwa wananchi kuwa na tahadhari ya juu.

MAONI YAKO