RAHEEM STERLING

Manchester City itamuuza mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling katika kipindi cha miezi 12 ijayo iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hatokubali masharti mapya ya kandarasi yake . Daily Mirror)

ARSENE WENGER

Aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger analengwa na shirikisho la soka nchini Japan kuchukua wadhfa wa mkufunzi mpya wa timu ya taifa. Raia huyo wa Ufaransa amesema kuwa bado ana hamu ya kuendelea na ukufunzi.. (Daily Mail)

GIANLUIGI DONNARUMMA

Chelsea imemuorodhesha kinda wa miaka 19 kutoka klabu ya AC Milan na kipa wa Itali Gianluigi Donnarumma katika orodha ya wachezaji wanaolengwa iwapo kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois,26, anayenyatiwa na Real Madrid ataondoka Stamford Bridge msimu huu. (London Evening Standard)

RICA KEYLOR NAVAS

Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 31, atasalia na kupigania nafasi yake ya kwanza katika klabu ya Real hata iwapo klabu hiyo ya Uhispania itamsajili Courtois. (AS)

DANIELE RUGANI

Beki wa Juventus na Itali Daniele Rugani, 23, atajiunga na Chelsea katika kandarasi ya miaka mitano yenye thamani ya pauni milioni 77,000 kwa wiki, huku Chelsea ikikubali kuwalipa mabingwa hao wa Itali dau la pauni milioni 44.2. (London Evening Standard)

DANY WARD

Leicester City imekubali malipo ya pauni milioni 12.5 na Liverpool kumnunua kipa wa Liverpool Dany Ward 25, na itakutana na mchezaji huyo wa Wales katika kipindi cha saa 24 zijazo. (Daily Telegraph)

TIMOTHY FOSU- MENSAH

Valencia inajiandaa kumsaini beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah,20, kwa mkopo kabla ya kumpatia mkataba wa kudumu. (Super Deporte)

MAONI YAKO