RAIS wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigali katika mapokezi ya Rais Nyusi na kutumbuizwa na ngoma asilia.THE NEW TIMES

KIGALI, RWANDA

RAIS wa Msumbiji, Filipe Nyusi, amewasili nchini Rwanda akiwa ni mgeni wa kwanza kati ya viongozi wengine mashuhuri wanaotarajiwa kuwasili nchini humo wiki hii.

Wageni wengine waliothibitishwa katika taarifa ya serikali ni pamoja na Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa India  Narendra Modi.

Akizungumza katika mapokezi ya Rais Nyusi na ujumbe wake, Rais Kagame alisema mataifa mawili hayo yanashirikiana katika majukumu yao na dira ya kuendeleza mapambano ya ustawi , usalama na utu wa raia wao.

Rais Nyusi, atakayekuepo Rwanda kwa ziara ya siku tatu, alipokelewa na Rais Kagame  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Kigali.

Mwaka 2017, Rwanda na Msumbiji zilisaini makubaliano ya pamoja katika maeneo ya kisiasa na ushauri wa kidiplomasia, kilimo, mifugo na uvuvi, uongozi wa umma, utalii, madini na utamaduni. THE NEW TIMES

MAONI YAKO