NAIROBI, KENYA

KILA habari zilizoandikwa kuhusu mrembo wa gereza la wanawake Lang’ata , Ruth Kamande,  zimekuwa zikieleza jambo moja kwamba alitenda kosa la mauaji na aliwahi kushinda taji la malkia wa urembo akiwa gerezani.

Gazeti la Daily Nation nchini Kenya limeweka bayana kuwa, jambo muhimu ambalo jamii haielewi kuhusu Kamande ni kwamba alipatiwa mafunzo ya Usaidizi wa sheria na alitumia ujuzi huo kuwasaidia wafungwa wenzake kuwaongoza katika mfumo wa sheria ambao mara nyingi umekuwa ukiwafanya waishie  mahakamani bila kuwa na wanasheria wa kuwaongoza.

Matokeo hayo huwafanya wengi wafungwe kwa kesi ambazo wanaweza kushinda kiurahisi wakati wangekuwa na wawakilishi wa sheria.

Kamande ni mmoja wa walionufaika na mradi wa  kujenga utu na matumaini ya jamii za magereza barani Afrika (APP), unaotekelezwa Kenya na Uganda kwa magereza ya Afrika, ambao hutoa mafunzo kwa wafungwa na walinzi.

John Muthuri, Meneja wa Msaada wa Kisheria ambaye alimpatia mafunzo Ruth Kamande kama ni Msaidizi wa Sheria alieleza kwamba,  alikuwa ni Msaidizi mzuri na walifurahishwa na kazi zake.

“Aliweza kujenga ujasiri na kujiamini kwa wenzake, akiwasisitiza kuzungumzia kesi zao kushinda kwa dhamana,” alisema.

Mradi wa APP kwa sasa unafanyakazi katika magereza manane nchini Kenya , pia mafanikio yamepatikana kupitia mpango wa Usaidizi wa sheria ambapo baadhi ya wafungwa waliofuata misingi hiyo,  wameweza kufika mahakamani na kufanikisha  hukumu zao za awali kubadilishwa.

Kwa mujibu wa APP, ingawa sheria inampa haki mwanasheria, asilimia 80 ya watu wanaoshutumiwa ambao wanafuata mfumo  wa sheria nchini Kenya hufanya hivyo bila kuwa na mwakilishi wa sheria na  hali hii husababisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha wafungwa. DAILY NATION

MAONI YAKO