NA HAFSA GOLO

MWAKILISHI wa jimbo la Mfenesini, Machano Othman Said, amesema misingi bora ya viongozi yenye kwenda sambamba na utatuzi wa kero za wananchi, itasaidia kuleta ushindi kwa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Alieleza hayo wakati  akizungumza na gazeti hili,katika tawi la CCM Kihinani.

Alisema kiongozi bora ni yule alie  mstari wa mbele kutimiza sera, ilani na ahadi alizozitoa kwa wananchi bila kufanya hiyana.

Kuhusu utekelezaji wa ahadi jimboni humo, alisema viongozi  wa jimbo hilo  wanaendeleza kutimiza ahadi zao kwa  wananchi hatua kwa hatua.

Alisema pamoja na juhudi zinazochukuliwa na viongozi hao katika uimarishaji wa maendeleo ya wananchi pia wanaendelea kusisitiza umoja na mshikamano  hasa ikizingatiwa ndio njia sahihi ya maendeleo na uhai wa CCM.

Sambamba na hilo alisema, atahakikisha matawi ya CCM yaliomo jimboni humo yanakuwa katika mazingira mazuri ili wanachama na viongozi waweze kufanya kazi za chama kwa ufanisi zaidi.

MAONI YAKO