NA MADINA ISSA

TAASISI ya Uongozi Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipago Zanzibar, imeandaa mdahalo kwa watedaji wakuu wa mashirika ya umma, sekta binafsi na asasi za kitaaluma, ukiwa na lengo la kuisaidia serikali katika juhudi za kujenga uchumi endelevu sambamba na kuimarisha maisha ya wananchi wake.

Akifungua mdahalo kuhusu nafasi ya maendeleo ya Zanzibar katika kukuza uchumi kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma, alisema pamoja na hatua zilizofikiwa katika kukuza uchumi bado umaskini unaendelea.

Alisema, mdahalo huo utasaidia katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii ambapo serikali itapata fursa ya kutathmini upya majukumu kama wakala wa maendeleo namna ya inavyotekeleza na sababu ya kuyatekeleza.

Aidha alisema kuwepo wataalamu kutoka nje katika mdahalo huo kutasaidia kuwapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu.

Alisema tokea mwaka 1964, serikali imechukua hatua mbalimbali kufanikisha maendeleo ya kiuchumi na ya jamii ambapo mingoni mwa hatua hizo ni kuruhusu mfumo wa biashara huria uliowezesha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi.

MAONI YAKO