NA MARYAM HASSAN

JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, linamshikilia Habesh Himidi (30) mkaazi wa Kikwajuni kwa tuhuma za kumpiga chupa ya kichwa Juma Kitiba (52).

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Haji Khamis Haji, wakati akizungumza na Zanzibar Leo ofisini kwake Madema.

Alisema kijana huyo mbali na kumjeruhi sehemu ya kichwa pia alimjeruhi shavuni na kumsababishia maumivi makali.

Alisema tukio hilo lilitokea Julai 8 mwaka huu Michenzani jumba nambari 7 na kueleza kuwa mtuhumiwa amefikishwa kituoni kwa hatua za kisheria.

Alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika lakini uchunguzi unaendelea.

Katika tukio jengine alisema katika maeneo ya bandari ya Malindi alikamatwa Hija Tno Mpemba (45) mkazi wa Kibei akiwa na karafuu polo tano na makonyo polo nne.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa wakati akiwa katika harakati za kusafirisha bidhaa hizo kwa ajili ya kuzipeleka Dar es Salaam huku akijua kuwa ni kosa kisheria.

MAONI YAKO