WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaaliwa Kassim Majaaliwa

NA AMEIR KHALID

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaaliwa Kassim Majaaliwa anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi katika sherehe za kijadi za Mwaka Kogwa Julai 18 huko Makunduchi.

Sherehe hizo ambazo hufanyika kila mwaka katika kijiji cha Makunduchi, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za tamasha la Mzanzibari, ambalo litafunguliwa rasmi Julia 19.

Ratiba ya tamasha hilo inaonyesha kuwa tamasha hilo litafunguliwa Julai 19 na kufungwa Julai 25 kwenye uwanja wa Gombani Pemba ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Abdalla.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa kuanzia tarehe hiyo ya ufunguzi kutakuwa na shughuli mbali mbali ikiwemo maonesho ya kazi za kiutamaduni viwanja Mapinduzi Square Kisonge.

Shughuli nyingine ambazo zitafanyika katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar ni Jukwaa la usiku wa Sanaa Julia 19 saa 2:00 usiku viwanja Mapinduzi Square Kisonge, Jukwaa na maulidi ya homu Ukumbi wa Haile Selaise Julai 21.

Julai 21 kutakuwa na kongamano la wasanii ukumbi wa studio ya Filamu Rahaleo,  saa 3:00 asubuhi, wakati Julai 22 kutakuwa na jukwaa la watoto saa 4:00 asubuhi viwanja vya Mapinduzi Square Kisonge, pia siku hiyo kutakuwa kongamano la wasanii na vijana uwanja wa Gombani Pemba.

Tamasha hilo litaendelea Julai 23 kwa kufanyika kongamano la vijana studio za muziki na filamu Rahaleo, Julai 24 kutakuwa na mchezo ng’ombe uwanja wa Gombani Pemba, na Julai 25 tamasha  litafungwa rasmi uwanja wa Gombani.

MAONI YAKO