BARCELONA,Hispania

UONGOZI wa Everton bado unafanya mazungumzo na mabingwa wa soka wa Hispania, FC Barcelona, kwa ajili ya kufanikisha uhamisho wa beki wa kati kutoka Colombia Yerry Mina.

Beki huyo aliacha gumzo nchini Russia kwenye fainali za Kombe la Dunia,  baada ya kuifungua Colombia bao muhimu wakati wa mchezo wa hatua 16 bora dhidi ya England na amekua kwenye rada za meneja mpya wa Everton, Marco Silva.

Meneja huyo anaamini endapo Mina atapatikana katika kipindi hichi cha kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya England, kikosi chake kitakuwa na kila sababu ya kuwa na safu bora ya ulinzi.

Uongozi wa Everton umesisitiza mazungumzo dhidi ya Barcelona yanakwenda vizuri na kuna matumaini makubwa ya kufikiwa makubaliano na kukamilishwa kwa dili la usajili wa beki huyo.

Mina amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona tangu aliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2017 akitokea Palmeiras.

Tayari wababe hao wa soka la Hispania wameshamsajili beki mwengine kutoka  Brazil, Arthur Henrique akitokea Gremio.(Goal).

MAONI YAKO