TURIN,Italia

KIUNGO wa Mcolombia, Juan Cuadrado, amekubali kiroho safi kumuachia jezi yake namba saba mchezaji mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo.

Cuadrado ndiye aliyekuwa anaitumia jezi hiyo.

Lakini baada ya kusajiliwa kwa Ronaldo akitokea Real Madrid, amelazimika kumuachia kutokana na umaarufu wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno.

Real Madrid imethibitisha kumuuza, Ronaldo kwenda Juventus kwa dau la euro milioni 105.

Ronaldo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na ‘bibi kizee hicho cha Turin’ ambao utagharimu euro milioni 30 kwa mwaka.

Aidha, klabu hiyo ilimshukuru mshambuliaji huyo ambaye anatambulika kuwa mmoja ya wachezaji bora dunia kwa miaka yote tisa aliyokaa santiago Bernabeu.(Calciomercato).

MAONI YAKO