HIVI karibuni dunia iliadhimisha siku maalumu ya kilimwengu ya kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya, ambapo kiukweli suala la mihadarati limekuwa tatizo kubwa la kiuchumi na kijamii duniani kote.

Vita dhidi ya dawa za kulevya vimekuwa vigumu sana kwenye uwanja wa mapambano, kwani inahusisha mitandao yenye kutumia fedha nyingi ambapo ni rahisi sana kumgeuza askari na kugeuka kuwa msaliti.

Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa usafirishaji wa dawa za kulevya duniani katika maeneo mbalimbali ya kikanda, unaendelea kushamiri na hivyo kuzidisha matatizo zaidi.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa, imeeleza kuwa eneo la Amerika ya Kati na Karibeani ndilo linaloongoza katika usambazaji wa dawa za kulevya hasa dawa hizo aina ya ‘cocaine’ na bangi.

Eneo hilo ndilo linalotumika kupelekea dawa za kulevya kwenda nchi za Amerika Kaskazini na Ulaya, aidha eneo hilo limeelezwa kuwa dawa za kulevya limeligeuza eneo hilo kuwa kinara wa mambo ya ukatili na kuwa na kiwnago cha juu cha mauaji duniani.

Ukiachilia eneo hilo, kwa mujibu wa ripoti, Amerika Kaskazini ndilo eneo linaloongoza kwa vifo vinavyotokana na matumizi ya dawa za kulevya hasa kutokana na watumiaji kuzidisha dozi.

Tani 15 zilizoangamiza za dawa za kulevya

MAONI YAKO