MWENYEKITI wa Baraza la Wauguzi, Amina Abdulkadri Ali, akizungumza katika siku ya wauguzi.

Asilimia 40 wanakimbilia kwa wakunga wa jadi

NA TATU MAKAME

SERA ya afya ya Zanzibar ya mwaka 1965 iliyofanyiwa mapitio 2011 inaeleza kuwa serikali itaimarisha huduma za afya kwa wananchi wote bila malipo. Na moja ya mkakati wa kuhakikisha sera hiyo inatekelezwa, serikali inaongeza bajeti ya afya kila mwaka. Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, bajeti ya afya imeongezwa kutoka shilingi 72.9 bilioni mwaka 2017/2018 hadi shilingi bilioni 108.5 mwaka 2018/2019.

Kati ya fedha hizo, shilingi 60.5 bilioni sawa na asilimia 65 ya bajeti ni kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma za afya katika hospitali za mkoa, wilaya na vijiji.

Pia imepunguza masafa ya kufuata huduma ya uzazi kwa wajawazito, ambapo vituo na hospitali 47 vya serikali na sita vya binafsi  vinatoa kutoa huduma ya kujifungulia huku nyumba za madaktari zikijengwa.

Hata hivyo, kuna mwitiko mdogo wa wazazi kuvitumia vituo vya afya kujifungua, wengi wanakwenda kwa wakunga wa jadi au wanakimbilia hospitali za wilaya.

Utafiti wa Wizara ya Afya Zanzibar wa 2014, umebaini asilimia 40 ya wajawazito Unguja na Pemba wanajifungua kwa wakunga wa jadi.

Tatizo la wajawazito kutovitumia ipasavyo vituo vya afya kujifungua lipo maeneo mengi, ikiwemo Bumbwisudi na Bogoa, ambapo wakaazi wa vijiji hivyo vilivyopo wilaya ya magharibi ‘A’ Unguja na wilaya ya Mkoani Pemba, hawavitumii ipasavyo vituo hivyo kujifungulia. Makala hii inajaribu kuangazia sababu zinazowafanya wajawazito kutovitumia ipasavyo vituo vya afya kujifungulia.

Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohammed, akizindua mkoba maalum kwa wajili ya wajawazito wanaokwenda hospitali na vituo vya afya kujifungua.

MAONI YAKO