Wafanya mkutano wa kihistoria Singapore

Unakifahamu walichojadili na kukubaliana?

JUNI 12 mwaka 2018, dunia ilisimama kwa muda pale fahali wa ulimwengu kutoka mashariki ya dunia Kim Jong Un na fahali wa magharibi ya dunia, Donald Trump walipopeana mikono kwa mara ya kwanza katika hoteli ya Capella iliyopo katika kisiwa cha utalii cha Sentosa huko nchini Singapore.

Huu ni mkutano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mamalioni ya watu duniani, kwani inaaminika kuwa unaweza kutoa picha kamili ya kuhakikisha amani na salama unadumu katika eneo la ghuba ya Korea.

Eneo la ghuba ya Korea limekuwa na hali tete tangu Korea mbili zilipopambana kwenye vita vya miaka mitatu kati ya mwaka 1950 – 1953, huku Korea Kusini ikisaidiwa na Marekani, ambapo hadi hii leo jeshi la Marekani limekuwepo katika ardhi ya Korea Kusini.

Tangu kumalizika kwa vita hivyo, zimekuwepo chokochoko na majaribio kadhaa ya kuhatarisha amani na kukaribisha vita kwa mara nyengine tena, hali iliyofanya dunia kuzitazama kwa karibu Korea hizo mbili.

Kutoka na uwepo wa wanajeshi wa Marekani ambapo hadi mwezi Agosti mwaka 2017 idadi yao ilikuwa 40,000, Korea Kaskazini imekuwa na hofu kubwa hivyo ili kuondokana na hofu hiyo lazima ijiweke tayari na kuwa imara kujilinda.

MAONI YAKO