RaisRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, akipata maelezo toka kwa Mfuti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally na Balozi wa Mororcco nchini Mhe. Abdellah Benyryane alipokagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waisalmu Tanzania (BAKWATA)

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amewataka viongozi wa dini kuwa wasemaji wa mambo yao na si kusemewa na wanasiasa.

Alisema hayo jana alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), unaojengwa Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alisema viongozi wa dini wanapaswa kuwa wasemaji wakuu wa mambo yao na si kuwaachia watu wengine ambao hawana uhusiano wowote na masuala ya dini.

Alisema kuwapa uwanja wanasiasa kuwa wazungumzaji wa masuala ya kidini kunaweza kulitumbukiza taifa katika hatari kwa kuwa wanasiasa wamekuwa na tabia ya kutaka kutumbukiza ajenda zao.

“Msitafute wasemaji kwa niaba ya maaskofu, mapadri, wachungaji, masheikh, kuweni wasemaji wa mambo yenu wenyewe. Mtakuwa mnatupoteza, taifa mtalipeleka kubaya. Mambo yenu yasemeeni wenyewe kuwapa watu wengine mtawachanganya wasikilizaji,” alisema.

Rais Magufuli alimkabidhi shilingi 10 milioni kwa Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeiry, zikiwa mchango wake katika kugharamia ununuzi wa saruji ili kuharikisha ujenzi wa msikiti huo unaotarajiwa kumalizika Aprili, 2019.

“Hela hii ikasaidie kununua mifuko 625 ya saruji ili msikiti huu ukamilike kwa wakati, nafahamu ujenzi wake unagharimiwa na Mfalme wa Morocco, lakini nami nimeona nichangie sehemu hiyo ndogo,” alisema.

MAONI YAKO