PARIS, Ufaransa

BRAZIL ndiyo taifa ambalo limeshinda mataji mengi zaidi ya Kombe Dunia ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2002. Waliandaa kombe hilo mwaka 2014, lakini, wakafungwa mabao 7-1 wakati wa nusu fainali na Ujerumani.

Hakuna taifa nje ya Ulaya au Amerika Kusini lililoshinda Kombe la Dunia, na ushindi kwa Ujerumani, Hispania na Italia katika fainali za mwisho tatu, ulimaanisha kuwa Ulaya inaongoza kwa mataji 11 dhidi ya 9 ya Amerika Kusini.

Mjerumani, Miroslav Klose anaongoza kwa kufunga mabao 16 kwenye mashindano manne ya Kombe la Dunia. Alistaafu mwaka 2016.

Mbrazil Ronaldo de Lima ni wa pili akiwa mabao 15 ambapo manane kati ya hayo o akiyafunga wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 2002.

Mfaransa, Just Fontaine ameweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye Kombe moja la Dunia. Alifunga mabao 13 kwenye mechi sita wakati wa mashindano ya mwaka 1958.

MAONI YAKO