RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,

NA MARYAM HASSAN

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sala ya Eid el- fitri, ambayo kitaifa itasaliwa viwanja vya Maisara mjini Unguja.

Hayo yalielezwa na Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Maliamana, Abdalla Talib, wakati akizungumza na Zanzibar Leo, ofisini kwake Mazizini.

Hata hivyo, alisema endapo siku hiyo itanyesha mvua sala hiyo itasaliwa katika msikiti Ijumaa Mwembeshauri.

Alisema sala hiyo inatarajiwa kusaliwa saa 1:20 asubuhi.

Aliwaomba waislamu kufika mapema katika viwanja hivyo ambapo takbira zitaanza saa 12:00 asubuhi ikifuatiwa na sala.

Alisema baraza la Eid linatarajiwa kufanyika ukumbi wa sheikh Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni ikiongozwa na Dk. Shein kuanzia saa 3:00 asubuhi.

MAONI YAKO